MRADI WA VIDEO YA ELIMU

KWA AJILI YA WATU WA MAKABILA YA DUNIA WAKIWEMO WATOTO NA VIJANA

Hii sinema ama filamu ya watu wa makabila ina nia ya kujenga hamasa na kuelimisha watu, wazee, vijana na watoto kuhusu masuala mbalimbali yanayotendeka duniani . Tunaweza kusema sinema hii ni masikio na macho ya jamii zetu kusikia na kuona yatendekayo mbali na jamii zetu. Filamu hii inatengenezwa kwa ukaribu na ushirikiano na watu wa makabila mbalimbali. Watu hawa wa makabila wametokea katika ngazi mbali mbali za maisha kama vile walimu,watemi,waga' nga, wafanyakazi wa mashirika ama washika nyadhifa mbalimbali katika jamii zao. Maono na ushauri wao unasaidia mradi huu na sinema hii kuona walipo tokea, mazingira yao pamoja na tamaduni zao. Kutokana na mchango wao mradi huu ama sinema hii inajenga chombo cha elimu kilicho beba sura za jamii zao.

Sinema hii imetengenezwa ili iwe rahisi kueleweka na rahisi kutafakari ujumbe. Kwa mwalimu wa makabila ,sinema hii ni chombo kizuri cha elimu kwa ajili ya watu wazima,vijana na watoto. Wasimulizi wa sinema hii ni walengwa wenyewe yaani watu wa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Lugha inayotumika katika kusimulia habari ya sinema hii ni Kireno, Kispaniola,Kiingereza,Kirusi and lugha nyingine za watu wa makabila

 

Walengwa wa sinema ama hadhira iliyokusudiwa:

Sinema hii imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya watu wa makabila wakiwemo watoto,vijana na wakina mama. Watu wengi wa makabila wanaishi maeneo ambayo ni vigumu kupata khabari mbalimbali muhimu zinazowahusu na kuwazunguka. Japo ni kweli sehemu nyingi watu wa makabila wanapoishi ni mbali lakini mara nyingi kuna sehemu karibu yao ambapo kuna uwezekano wa kuona sinema ama kusikiliza redio. Kwa mfano makanisani, ama kwenye ofisi za mashirika au hata ofisi ya viongozi wa kijiji. Sehemu hizi zaweza kutumika kwa ajili ya kutoa ujumbe huu muhimu.

 

Malengo:

 • Malengo ya sinema hii ni kama yafuatayo
 • Kuwaonyesha walengwa kwa njia ya picha ama sauti utajiri wa utamaduni na mazingira, walio nayo makabila ya dunia kwa pamoja
 • Kuelezea kuhusu masuala,matatizo na mapambano ya watu makabila na kuonyesha kila jamii ya makabila ina matatizo yanayo shabihiana
 • Kuelezea mbinu za kutetea na kushawishi ili kuleta mafanikio juu ya matatizo walio nao jamii za makabila
 • Kujenga ushirikiano na mtandao ili kuimarisha malengo na mikakati
 • Kuwamasisha makabila kujumuika katika ngazi ya mikoa,taifa na kimataifa. Hii ni katika azma ya kuwezesha makabila kuelezea masuala yanayohusu maisha yao na kujiamua masuala yao wenyewe
 • Kujenga uwezo wa jamii husika katika kutafsiri maana ya maendeleo,utamaduni na masuala mengine nyeti

 

Muundo wa Sinema ya kielimu

1. Ramani ya dunia:
Dunia kwa mujibu wa Jiografia Maumbile
 • Tufe
 • Ramani
 • Ramani inayo onyesha sura ya nchi
 • Mabara
 • Nchi
2. Vielelezo vya mazingira asili
Film clips with musical accompaniment
 • Bahari
 • Afrika
 • Antantika
 • Asia
 • Ulaya
 • Australia
 • Amerika ya Kaskazini
 • Amerika ya kusini
3. Masuala ya mazingira yanayohusu dunia kwa ujumla
Vielelezo ambayo vitasimulia kuhusu masuala ya kidunia ya mazingira na athari zake katika sayari yetu
 • Miradi isiyo endelevu kama uvunaji wa miti, migodi na malisho ya mifugo
 • Uchafuzi wa vianzo vya maji,hewa,bahari na ardhi
 • Miradi mikubwa ya maendeleo kama mabwawa,barabara,uchimbaji mafuta na gesi
 • Ongezeko la watu
 • Ongezeko la joto duniani
 • Tabaka la ozone kuathiriwa
 • Uvuvi haramu na usio endelevu
 • Upotevu wa bionuwai
 • Kupotea kwa tindiga,misitu na vyanzo vya maji
 • Utafiti wa Kisayansi unaolenga katika kubadilisha maumbile asili ya mimea na wanyama
 • Utandawazi
4. Sinema ama video kutoka kwa makabila yenyewe
 • Vielelezo kutoka kwa walengwa wenyewe kwa utaratibu wa bara hadi bara
 • Mfano wa muziki asili kutoka kila bara mfano Afrika
 • Sinema hii itakuwa katika lugha ya kienyeji kwa mfano Kiswahili,Kirundi ama Kimasai
5. Masuala ya kisiasa yanayohusu jamii za makabila
 • Uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe
 • Umilikaji ardhi na maeneo
 • Haki ya kujipatia maendeleo
 • Uharibifu mazingira,uchafuzi na uwajibikaji
 • Miradi mikubwa ya maendeleo na athari zake juu ya maisha ya wenyeji ama makabila
 • Kutambuliwa kwa makabila na serekali
 • Kuanzishwa kwa sheria za kitaifa na kimataifa na utekelezaji wake
 • Utandawazi
 • Kutozingatia mikataba kwa serekali
 • Ukandamizaji kwa njia ya utamaduni
 • Ubaguzi
 • Uchumi, Jamii, Siasa, Urithi wa Utamaduni, Haki miliki, Elimu ya kiasili, Rasilimli za Kigenetiki, haki binafsi na haki jamii
6. Mbinu za makabila
Mfano wa vielelezo na masimulizi ya watu wa makabila katika kuelezea ama kutatua matatizo yao
 • a) Mazingira

 • Ukususanyaji wa vielelezo,upimaji ramani wa maeneo na usimamizi wa matumizi ya maliasili
 • Kulinda na kutunza masingira kwa mfano kuanzisha bustani ya miche ya miti
 • Kujenga kituo cha kutunza wanyama walio hatarini kwa azma ya kuwarudisha sehemu zao asili
 • Kulinda na kulinda mebegu asili
 • Kukusanya na kuandika takwimu juu ya matumizi ya mimea na mbinu za upandaji mimea
 • Kitengo cha elimu na mazingira cha makabila
 • b) Siasa

 • Kuwa na uwezo wa kutafsiri maana ya masuala mbalimbali yanayowahusu walengwa na kujumuika katika kuamua mambo yanayo walenga
 • Kushiriki kisiasa katika nyanja zote kama vile kijiji,wilaya,mkoa,kitaifa na kimataifa
 • Ujengaji uwezo
 • Ujengaji mtandao na ushrikiano
 • c) Elimu
 • Kuwezesha aina mpya ya elimu ambayo ina vipengele vya kisasa pamoja na ya kiasili ambayo itasisitiza kutunza,kuanzisha na kubakiza utamaduni kama vile sanaa,lugha,siasa,elimu asili yaani iliyo andikwa na isiyo andikwa.

 • Ukusanyaji taarifa ama khabari na kutoa tathmini juu ya masuala mbalimbali
 • Ukusanyaji taarifa, kupima ramani na kutoa tathmini juu ya masuala ya sasa na zamani ya kimazingira,kitamaduni na kijamii
 • Kushirikiana na kubadilishana elimu na uzoefu kati ya jamii za makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi ama bara. Hili zoezi litawahusu walimu na watu wengineo
 • Uchapishwaji wa vitabu katika lugha mbalimbali . Yaliyomo katika vitabu yatatoka kwa wazee na vijana wa maeneo husika
 • d) Utamaduni
 • Utunzaji wa tamaduni za wahenga ama mababu:

 • Ukusanyaji wa habari na elimu ya kiasili na utamaduni
 • Shule zenye kufundisha lugha mbili kwa mfano kiingereza pamoja na Kisambaa ama Kihadzabe
 • Kutoa hamasa na kujenga mori juu ya utamaduni na urithi
 • e) Afya
 • Usimamizi wa masuala ya kiafya ya jamii

 • Kwa kutumia elimu , kuwezesha utoaji wa huduma za afya ndani na nje ya jamii. Pia kuwezesha utabibu wa kisasa kama ikihitajika
 • Ukusanyaji wa taarifa ama khabari ya madawa ya kiasili, utengenezaji na uvununaji. Pamoja na kujenga hamasa juu ya matumizi ya madawa ya kiasili
 • f) Vyombo vya habari
 • Indigenous media projects and programs

 • Sinema na video
 • Sanaa
 • Uandishi habari
7. Uboreshaji wa Haki
 • Nini umoja wa mataifa na shughuli zake
 • Watu wa makabila na umoja wa mataifa
 • Sehemu nyingine ambapo malalamiko yanaweza kutolewa
8. Collective global responsibilities as Earth Peoples
Hata kama tunatokea katika tamaduni na jamii tofauti , sisi bado ni watu wamoja na tunaishi katika hii sayari iitwayo dunia. Kwa mantiki hiyo, sisi tuna wajibu juu ya masuala ya sayari yetu. Kuna mianya mingi tunayo weza kutumia ili kubadili mwenendo wa sasa wa dunia ambao hauna uendelevu. Imani hii itawezesha uhifadhi wa maliasili na tamaduni zetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 • Sababu na athari itokanayo na matendo ya binaadamu na ulafi
 • Haki za binaadamu

 

Translated by Khalfan Mohamed and Mohamed Yunus