MUUDO WA MRADI WA VIDEO

 

Mradi huu utahakikisha kwamba unalinda ahadi iliyotolewa kwa washirika wake ambao wamejiunga na mradi huu wa video. Mradi huu na Earth People wanafanya kazi kwa kuaminiana na kwa uwazi na kwa lengo kwamba juhudi za pamoja zitapelekea kupatikana kwa mkanda wa video ambao utakuwa kwa ajili ya kuelimisha jamii na kupashana habari, usio na madhumuni ya kupata faida, na ambao utatengenezwa na kufinyangwa na wahusika wenyewe, yaani jamii za makabila.

 

KUHUSU WASHIRIKA WA MRADI

Washauri MahususiKutakuwa na washauri mahususi ambao ni wataalam na wajuzi katika nyanja husika na watatoa mchango wao katika mradi

WashirikaKutakuwa na washauri mahususi ambao ni wataalam na wajuzi katika nyanja husika na watatoa mchango wao katika mradi Kwa upande wa washirika wao wana jukumu la kukusanya habari mbalimbali kama vile mikanda ya video ya maeneo yao, muziki n.k. Washirika watakuwa wakijadiliana mara kwa mara na jamii zao kuhusu maendeleo na hatua za mradi. Washirika hawana budi kuwafahamisha mara kwa mara jamii zao kuhusu maendelo ya mradi, kuwahamasisha na kujadiliana. Pia ni wajibu wa washirika kuwa kioo cha jamii zao ama mashirikayao, kutafsiri video katika lugha zao za kienyeji na pia kusambaza video wakati itakapokamilika.

A Baraza SimamiziKutakuwepo na baraza simamizi ambalo litakuwa limeundwa na walengwa yaani jamii za makabila na wanaharakati wengine ambao watahakikisha mradi unakwenda mbele, hawa ni watu wenye ujuzi kuhusu masuala mbalimbali ya makabila. Itakuwa kazi ya baraza simamizi kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu maeneoyaona ujuzi walionao katika nyanja fulani.

MASAWASILIANO

Ili kuboresha mawasiliano, Earth People imetumia njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo kutumia mtu kupeleka ujumbe ama habari kwa mhusika, sanduku la posta, redio, simu, mtandao na barua ya kipeperushi. Hii ni kuwezesha mawasiliano na washrika wa mradi wetu ambao wamesambaa kila pembe ya sayari yetu.

Mtandao wa website wa Earth People unataka kufanya kazi kwa uwazi na washirika wake, hivyo basi , kila mshirika atapewa namba ya siri ambayo itamwezesha kuangalia habari mbali mbali katika mtandao kama vile historia fupi ya kila mmoja wa washirika, makala, picha, anuwani, kitengo cha mazungumzo kwa njia ya mtandao, vipande vya video na sauti na habari mpya kuhusu maendeleo ya mradi.

 

USAMBAZAJI

Usambazaji utakuwa katika hatua nne:

  1. Katika hatua ya awali, vipande vifupi vya video vitapatikana kwenye mtandao wa ERATH PEOPLES.
  2. Katika hatua ya pili, video ambayo bado iko kwenye matengenezo itasambazwa kwa washirika kwa ajili ya maoniyaona yale ya jamii zao ama mashirika.
  3. Katika hatua ya tatu, video ambayo imesha kamilika na kuhaririwa yenye masaa mawili na nusu itaonyeshwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa baraka na ushirikiano wa watu wa makabila wa dunia.
  4. Katika hatua ya mwisho, video iliyokamilika itatumwa kwa washirika wote wa mradi, mashirikayao, walimu wa makabila na jamii zao. Usambazaji wa video utakuwa jukumu la washirika wetu ambao wataonyesha video hii kwa jamii zao pamoja na kushirikiana na walimu wa makabila, wanaharakati, mashirika, jamii. Video hii pia inaweza kuonyeshwa kwenye vituo vya taaluma, mikutano, kwenye masoko ama magulio na sehemu zingine za makutano.

Tunahimiza jamii husika kupiga kopi na kusambaza mkanda huu wa video katika maeneo yao. Ujumbe kwenye mkanda huu wa video kwa jina la Earth People utakuwa bure.

 

Translated by Khalfan Mohamed and Mohamed Yunus