TAMKO LA NIA YETU

Earth Peoples [Watu wa Ardhi] ni jumuiya wa wazee, akina mama, akina baba,vijana, viongozi, wanaharakati,waalimu pamoja na mashirika madogo madogo na makubwa, yote yameungana pamoja kwa nia kuboresha na kutetea mazingira na haki za watu wa makabila.

Nia yetu ni kutengeneza video ya kielimu ambayo itakuwa chombo cha kushirikiana,kubadilishana na kusambaza habari na rai kuhusu masuala mbalimbali nyeti katika jamii za makabila pamoja na dunia kwa ujumla.

Kwa kupitia shughuli zetu , tutawezesha jamiii za makabila kushika hatamu ya maendeleo yao na kuwapa nafasi ya kutoa maamuzi na rai maana masuala mengi yanayo wahusu watu wa makabila yanakaribiana na mienendo ya sasa ya kiduniya.

Ni nia yetu pia, kusherekea na kutoa heshima kwa utajiri maridadi unaopotea wa Mama Yetu Dunia, kwa kuonyesha mchanganyiko na utajiri mkubwa wa mimea na wanyama. Tutahimiza utunzaji wa mazingira na heshima kwa wanyama na mimea.

Translated by Khalfan Mohamed and Mohamed Yunus