JIUNGE NASI

 

Azma yetu ni kutengeneza sinema isiyo ya kibiashara kwa ajili ya jamii za makabila kila mahali walipo hapa duniani. Sinema hii yenye kugusa mada mbalimbali na kuelimisha jamii itaitwa Earth Peoples (Watu wa Dunia / Ardhi). Sinema hii ya Watu wa Ardhi imefinyangwa na kutengenezwa kwa juhudi ya washirika na washauri kutoka pembe zote za dunia.

Tunatoa wito kwa kila mtu kujitokeza mbele kwenye mradi huu na kuchangia mawazo, maoni, rai na hekima ili kuweza kutunza mdundu wa jadi wa makabila yetu, kwa kutumia vyombo vya habari vya kisasa ili kuweza kujenga na kuimarisha jamii zetu.

Chukua muda kusoma yote yalioandikwa kuhusu Mradi wa Sinema ya Makabila na kama unaona ni mradi mzuri naomba utujulishe.

join us